Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara kumutanisha Tabulele na Diamond

Diamond Mweh Ms Tabulele Manara kumutanisha Tabulele na Diamond

Fri, 1 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyekuwa msemaji wa Klabu ya Yanga, Haji Manara amesema kuws atamkutanisha Msanii David Riger @riger_tabulele aliyeimba wimbo wa Tabulele na Msani Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' ili wafanye ngoma.

Manara amekutana ma msanii huyo kutoka Congo katika ofisi za Manara TV Posta, Jijini Dar es Salaam na kumpa ahadi hiyo.

"Huyu lazima afanye dude moja na Diamond Platnumz. Kwanza nitawakutanisha na kuona jambo hilo linatokea kabla hamjarudi kwenu Congo, huwezi kuja Dar es Salaam halafu ukawa hujaonana na mimi au Diamond Platnum. Sisi ndiyo mastaa wa Jiji hili," alisema Manara.

Msanii huyo ameletwa nchini na Yanga SC baada ya kutoa wimbo huo uliowateka mashabiki wa timu hiyo.

Riger tayari ameshakutana na supastaa wa Bongo Fleva, Harmonize na inaelezwa huenda wakawa na mikakati ya kuachia ngoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live