Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara amwagia sifa ka'zote mchumbake Zaiylissa

Manara Na Zayllisa Manara amwagia sifa ka'zote mchumbake Zaiylissa

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Marehemu Babu yangu Mzee Omari Saidi Mkivya Mzaramo wa kazimzumbwi ( Mungu amrahemu) aliwahi kuniambia wakati naoa ndoa yamgu ya kwanza kabisa ( Mama yao kina Hamida ) mpe furaha sana mkeo hata kwa kidogo chako.

"Make sure everyday unamnunulia hata zawadi ya Pipi, Msifu sana sirini na hadharani, mpe maua yake na mfanye kama Yai la Njiwa" Marehemu Babu ambae ujanani kwake aliitwa Rock&Roll na alikuwa Dereva Taxi maarufu mjini, alinisisitiza mpe good time na ukijaaliwa mtoe sana outing na ikibidi Vacations ziwepo za kutosha!!

Namwangalia Rihanna wangu ,nasema na kuahidi mbele yenu, Zai atakuwa ni miongoni mwa Wanawake wenye furaha zaidi kwa kufata yote aliyokuwa akiniusia Babu yangu huyo ambae baadae aliangukia sana kwenye dini.

Sina utajiri wala sina uwezo mkubwa,lakini yale maelekezo ya Rock&Roll,Alhamdulillah namshukuru Mungu nayamudu,si haba.

Nb: Mimu mwenyewe sijui naoa lini ila nnachojua wiki hii haiishi InshaAllah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live