Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara amuomba Diamond kupiga shoo ya kibabe Yanga

Diamond Manara Bn Diamond na Manara

Fri, 17 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Young Africans, Haji Sunday Manara amemuomba supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz kuangusha shoo ya kihistoria wakati wa sherehe za kilele cha Wiki wa Wananchi.

Ombi hilo la Manara linakuja ikiwa ni siku moja baada ya Yanga kutwaa ubingwa wa 28 wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kuifunga Coastal Union bao 3-0 huku Diamond akimpongeza Manara na Yanga kwa ujumla na kusema anafahamu figisu nyingi alizofanyiwa Manara akiwa Simba lakini hawezi kuzisema hadharani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara ameandika; "My Blood umeendelea kuwa na mimi katika kila hali, iwe ya huzuni au ya furaha kama niliyonayo sasa.

"Wewe ni Rafiki wa kweli na usiye na haya katika kuwasemea ndugu na rafiki zako, huna unafik na huna khulka za Waswahili wengi wanaopenda kujitia kubalance balance vtu, ili waonekane wema kila upande.

"Kwako kitu YES utasema YES na NO ni NO tu, huna kumwangalia Mtu usoni Kwa sababu yoyote ile, but hizi ni sifa za Watoto wa kidarisalama, ambao kwao wao Maisha ni Part ya kifo tu.

"Ndioooooooooooo, Mwamba tuombe uhai tu, lakini Kilele cha Wiki ya Wananchi inakungoja wewe Mwanamme, Tunatarajia Show kubwa zaidi kuwahi kufanyika Tanzania, toka tupate Uhuru.

"NB: Tajiri kaniambia nikuombe hadharani,, Utupe Songi moja matata la Ubingwa, na c unajua sisi hatuna Chupli? Au Wananchi mnasemaje? Weka maneno tustue nchi kidogo. Beauty Beauty @diamondplatnumz," ameandika Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live