Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Manara amshauri Diamond kuoa, amponda Dimpoz

MANARA DIAMOND DIMPOZ Manara amshauri Diamond kuoa, amponda Dimpoz

Thu, 29 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Yanga, Haji Manara amemshauri msanii Diamond Platnumz kufunga ndoa kwani umri aliokuwa nao ndiyo umri mzuri zaidi kwa ajili ya kuingia kwenye maisha ya ndoa.

Manara ameyasema hayo huku akizungumzia manufaa ambayo msanii huyo atayapata baada ya kufunga ndoa, ikiwemo kuongezeka kwa utulivu na ufanisi kwenye kazi zake na hii ni kutokana na tabia yake ya kupenda kujituma na kufanya kazi zaidi.

akimzungumzia Ommy Dimpoz, Manara amesema; “Ommy Dimpoz hawezi kuoa kwasababu atapata tabu sana kuishi na mwanamke kutokana na yeye kujipenda sana na kuwa msafi mno kupitiliza, anapenda kuoga mara nyingi, anapenda kuvaa nguo sana na kubadilisha.

"Dimpoz anatumia muda mwingi kwenye kujiangalia na kujitayarisha anapokuwa anajiandaa zaidi hata ya mwanamke, hakuna mwanamke ambaye atakaa naye na kuweza kumvumilia” alisema Manara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live