Haji Manara alikuwa na haya machache kuhusu issue ya Achraf Hakimi na mke wake ambaye ni mwigizaji Hiba Abouk, Haji ameandika,
Kwangu mimi huyu ndio Mwanamme Shujaa zaidi toka mwaka huu umeanza, ana maono ya mbali na ametupa fundisho kubwa mno.
Niliwahi kushuhudia miaka ya nyuma Mtu kamnunulia Mkewe Gari nzuri mpya lakini siku chache tu baadae demu kapeleka file la Gari nyumbani kwao, kesi ile ilipokuja kwangu kama rafiki nikajiuliza kama Gari tu, inakuwa hivi je Mali kubwa kubwa itakuwaje?
Asilimia Tisini ya Wanawake wanaoolewa na Watu maarufu hawana mapenzi ya kweli, wengi wao wanatamani ile fame ya Mwanamme, wapo pale kutaka kuwa maarufu na wao.
Wanaenjoy kuandikwa mitandaoni na wanazifurahia zile moments za Camera zinazomfata mumewe na yy , ndio maana aina hii ya Wanawake sio ajabu kufanya lolote kuendelea kuandikwa mitandaoni, na kwao kuiba vitu vya mume na kuondoka navyo wala sio shida zao.
Kwao Mali ndio everything, kwao umaarufu ni alfa na omega, wanalosahau umaarufu ni wa mume sio wao , utaupata katika kipindi kifupi mno, baadae utaisha na atabakia nao Mwanamme aliyehasle kuutafuta.
Imagine huyo demu wa Hakim alivyo maarufu now kwa ujinga wake,blakini soon shujaa ataendelea kuwa Mwanamme na yeye atapotea mazima kama walivyopotea Wanawake wengine wapumbav kama yeye.
Mali kakosa na umaarufu utaisha soon.
Kwao wao ,,,mama zao ni kila kitu, ila Mwanamme akiwa karibu na Wazazi wake au ndugu zake hawapendi.wanataka wao wapewe thamani kubwa kuliko mama zetu,,wengine hununa hata kwa vizawadi kidogo tu kwa mama waliotuzaa na kutulea,,
Ingawa nieleweke sio Wanawake wote wana tabia hizi, lakini wengi wao kwa Watu maarufu wanafata vimali vyetu tulivyoomba navyo Mungu na umaarufu tu.uzuri wa umaarufu wao ni wa muda mfupi mno,,baadae wanajitilisha huruma DM
Jiulize kitu kimoja,,kabla ya huu umaarufu walikuwa wapi hawa Janjaweed?