Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Man X: Sisikilizi nyimbo za Diamond

Man X Man X: Sisikilizi nyimbo za Diamond

Sat, 30 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva Man X amesema kuwa pamoja na kuwa nje ya game kwa muda mrefu na kutambua mabadiliko ya muziki lakini bado haukubali mziki anaoimba Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz kwa sababu ngoma zake hazimuingii kichwani.

Akihojiwa, Man X amesema mara nyingi anapenda kusikiliza ngoma kutoka Uingereza kwasababu kuna vitu anataka kujifunza kuhusu ngoma za wasanii wa ndani amebainisha kuwa hawa wapo tu.

Alipoulizwa kuhusu wasanii anaowakubali hapa nchini amewataja Profesa Jay, Sugu, Afande Sele, AY pamoja na Dully Sykes.

Aidha, amewataja wasanii ambao wanatakiwa kuheshimiwa kila siku kutokana na mchango wao kwenye tasnia ya muziki nchini ambapo amewataja Profesa Jay, Sugu, P- Funk, Master Jay pamoja na Bizman.

Sambamba na hayo Man X ametangaza kuachia ngoma yake mpya ya Nyepenyepe huku akisisitiza kuwa amerudi rasmi na anaomba mashabiki wa muziki wa Bongo Fleva wampokee katika ujio wake mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live