Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo yazidi kuiva Mdundo wa Taifa

Basata Mdundo Wa Taifa Mambo yazidi kuiva Mdundo wa Taifa

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya mdundo wa Taifa tarehe 26 Septemba, 2022 imekutana katika ukumbi wa bodi ya filamu chini ya uenyekiti wake Dkt. Kedmon E. Mapana kisha kubainisha midundo ya makabila itakayoweza kutumika kupata mdundo wa Taifa.

Aidha, kamati hiyo imekubaliana kukutana na wadau mbalimbali ili kupata maoni na vionjo vitakavyoboresha mdundo wa taifa.

Katika hatua za awali kamati hiyo imefanikiwa kupitia sampuli za midundo zilizobainishwa na kila mwanakamati ili zisaidie "creators" kufanya kazi yao kwa urahisi zaidi.

Kwa sasa wajumbe wa kamati hiyo wanaenda katika maeneo mbalimbali nchini kukutana na wadau wa muziki ili kukusanya maoni yao yatumike katika kutengeneza mdundo wa taifa unaotarajiwa kukamilika hivi karibuni.

Kamati ya mdundo wa taifa iliundwa na kuzinduliwa na Mhe. Mohamed Mchengerwa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo mnamo mwezi Julai mwaka huu ikijumuisha wabobezi mbalimbali kwenye tasnia ya Sanaa hapa nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live