Jamii inawachukulia poa na kuwadharau Baba Levo na Mwijaku. Sikatai, kuna kila sababu ya kuwasema vibaya.
Nimekuletea hapa Mambo 10 ya kujifunza namna ya kuji-brand kutoka kwa hawa majamaa.
1. Polarization and Neutrality ni vitu hawa majamaa wamefanikiwa sana. Ukifanya baya watu watakupokoa, ukifanya jema bado utakula spana. Fanya utakalo.
Watu wanapenda kuwa neutral kwa kuogopa kuwa against watu wengine, Mwijaku leo anampiga spana Diamond, kesho Konde. Baada ya wiki unasikia Wasafi Bet imempa Mwijaku dili.
Kuna madili utayapata kwa kuwa upande wako na kuupinga upande mwingine. Kuna watu wengi wana mtazamo kama wako ambao watakusupport na kukubali daima. Never be neutral????.
2. Maisha ni mchezo wa karata Sukuma karata dume pekee. Hawa jamaa walisoma gemu na kushika karata ya uchawa. Hii ni karata ambayo kwao imekubali.
Wote tuna karata zetu, wengine wanasukuma kwa woga, kuogopa macho ya watu. Be you.
3. The Power of Compound Effect Hawa jamaa ni maarufu sana, hasa IG. Kila uchao wanaongeza followers na fans. Utake usitake.
Na nature inaendelea kuwakubali kwa kuwaletea watu na madili zaidi. Tutumia mbinu zao za kichawa kujenga mishe zako. Hutaki. Baki na ego yako.
4. Attention is the new currency Attention itafanya watu waaamini mavi ya mbuzi kuwa ni karanga.
Hata kama mwonekano utabaki kuwa ni mavi ya mbuzi bado kuna watu wataonja kujiridhisha kama ni kweli.
Kama unajenga biashara ama brand yako, saka attention kadri unavyoweza Top G anasema hakuna attention mbaya.
5. Tafuta attention, leverage ili uweze kupiga pesa kwa watu kukufuatilia.
Utakubaliana na mimi kuwa Mwijaku na Fundi majumba ni mafundi kweli kweli wa kutengeneza attention na daima kukaa midomoni mwa wafuasi wao.
6. Kutokuogopa macho ya watu ni somo kubwa sana Haimaanishi na wewe ujitoe fahamu.
Kama unaweza kudance. Dance. Ukikikalia talanta, utalala njaa. Wale unaowaogopa hawatakuwepo pale bills zako zitakapokuwa zimekukalia shingoni.
6. Go out and shine.
Kusimamia kile unachoamini na pale mambo yanapobadilika kukubali ulikosea Kuna watu ukiwauliza swali jepesi tu watakimbilia kuwa neutral.
Hofu yao ni vipi mambo yakija kugeuka hapo baadae. Wewe ni binadamu kama binadamu wengine. Kukosema ni ubinadamu Kama unajua jambo fulani toa mtazamo wako.
Mambo yakibadilika kubali haukuwa sawa, na unakubaliana na hali ilivyo sasa.
7. Hakuna atakaekuja kukupiga.
Jiamini kwa yale unayoyafahamu na ishi kama wewe bila kufuata upepo kwa watu wengine.
Usiogope kutofautinana na mtu, wakati mwingine ndo nafasi ya kwenda juu Wengi tunafahamu kuwa Mwijaku huwa anamkubali sana Konde hata kama anakula pesa za Wasafi.
Kwa akili ya kawaida mtu utaogopa kuonesha kumdiss Diamond wazi ukidhani atakuchukia kumbe diss zako zina faida kwa jamaa.
Ndo maana Mwijaku anakula mashavu Wasafi na ukweli ni kwamba jamaa huwa anamsulubu sana Boss wa Wasafi kwenye mambo mengi especially upande wa muziki.
8. Usiogope kuwa tofauti.
Kama una talent kubwa na jamii haijui, hiyo talent ya nini kama haileti ugali mezani⁉️
Kuna watu wana uwezo mkubwa sana lakini wamejifungia majumbani mwao. Kuna watu wana bidhaa nzuri sana, lakini hawatoki kupiga kelele.
Kila chembe ya nukta ni fursa ya kuukimbia umasikini Usiwe mtu wa kuogopa kujaribu vitu.
9. Kuna vitu vingine huja kama mchezo kumbe ndo fursa zenyewe.
Ukiipata shikilia kama Baba Levo na Diamond. Usikubali watu kukutoa mchezoni.
Binadamu wanafiki sana Watakuja kukupiga spana na kukukatisha tamaa.
Cha ajabu wanakufollow.
So, don’t consume their negative energies.
Push agenda yako kwa 100%.
Hakuna atakayekuja kukuokoa au kukusaidia.
You are 100% responsible for your life.
NB: Huu ni mtazamo wangu.
Nimejifunza kuangalia yaliyo mema kwenye kila jambo.
I only see and talk positive energy.
Unachoweza kufanya ni kujifunza hizi mbinu za kichawa na kuwa chawa promax kwenye hustle zako. Period.