Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mambo matatu ya kutofanya katika kipiindi hiki cha sikukuu

89539 Xmass+pic Mambo matatu ya kutofanya katika kipiindi hiki cha sikukuu

Mon, 23 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Tunakumbushana tu, sikukuu maana yake ni sherehe, kufurahi na kula raha ambazo labda ulizikosa mwaka mzima na hiki ndiyo kipindi chake.

Sasa ili mwanaume ufurahie sikukuu yako, tunaamini kuna mambo unatakiwa kuyafanya na mengine ambayo hutakiwi kuyafanya. Leo tuzungumzie matatu ambayo hutakiwi kuyafanya.

Usianze uhusiano mpya

Kama kuna jambo hutakiwi kulifanya katika kipindi cha sikukuu ni kuanzisha uhusiano mpya wa mapenzi. Kipindi hiki huko nje karibu kila mwanamke anatafuta mdhamini wa kuishughulikia sikukuu yake. Mdhamini wa kumpeleka saluni, kumtoa auti, kumnunulia simu mpya nzuri za ofa kutoka mitandao ya simu na wa kumpa pesa kizembe.

Hii ni sawa na kusema, ukijiingiza kwake tu, wewe ndiye utakayepewa jukumu hilo na itakubidi utimize kama ambavyo kuna jambo unataka na yeye akutimizie hiyo ni moja.

Pili ni kwamba, uhalisia unaonyesha kuwa wanaume wengi tunatumia pesa kwa kiasi kikubwa sana kwenye mahusiano mapya ili kuwaonyesha wenza wetu kwamba na sisi tupo. Sasa hii ni sawa na kusema, utumiaji wa pesa utaongezeka mara mbili kwa sababu upo katika kipindi unachohitaji pesa yako itumike kujionyesha.

Hii tunaisema kwa kurudia kwa sababu ni muhimu sana. Si kila meseji ni ya kujibu kipindi hiki cha sikukuu. Mwanamke akikutumia meseji inasema ‘Baby nikwambie kitu?’ usiijibu hiyo meseji.

Ukijisumu ukajibu unarudishwa kwenye mambo tuliyoongea hapo juu. Utaombwa pesa ya saluni, simu mpya, hataki kuanza mwaka na simu ya zamani, anataka umpeleke sehemu akafurahie sikukuu, kuimwagia pesa sikukuu yake. Na kama mwanaume hutakuwa na cha kufanya zaidi ya kumtimizia tu.

Usikope tena

Kwa sababu kwanza wengi wetu matumizi yetu hufanana na pesa tuliyokuwa nayo karibu au tuseme mkononi. Ukiwa na Sh20,000 utajikuta tu unaishi vivyo hivyo ukiwa na Sh500,000.

Sasa ni bora kula sikukuu kwa pesa uliyonayo lakini ukawa huru, huna madeni, kuliko kula sikukuu kwa pesa ya kukopa, cha ajabu ukishaikopa utashangaa kuna majukumu yatatokea kusikojulikana na utalazimika kuyashughulikia kwa pesa hiyo hiyo ya kukopa, matokeo yake inaweza isitoshe.

Lakini pia, kila siku tunaambiwa tusikope kwa ajili ya anasa. Ukikopa kwa ajili ya sikukuu maana yake ni pesa yako ya mwezi ujao umeshaitumia, tena ndani ya saa 24 tu, mwezi ujao itakubidi ukope tena ili kujazia kile ulichopunguza katika matumizi ya sikukuu.

Hii maana yake ni kwamba unaweza kujikuta mwaka mzima unahangaika kulipa deni moja ambalo labda usingekutana nalo kama ungeamua kufurahia sikukuu kwa pesa iliyopo mfukoni mwako.

Chanzo: mwananchi.co.tz