Machi mwaka huu mbwa wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu aitwaye Vanilla au Manunu aliteka mazungumzo hasa mtandaoni mara baada ya Wema kutangaza dau la Sh2 Milioni kwa yeyote atayempata mbwa wake ambaye aliyetoweka nyumbani.
Lakini mbwa huyu ni wa aina gani na kwanini amekuwa akipewa kipaumbele kiasi hiki?. Haya ni mambo 10 usiyofahamu kuhusu mbwa huyo wa Wema.
1. Kwa kawaida mbwa Manunu hupelekwa saloni kwa ajili ya usafi na kuboresha muonekano wake walau mara mbili kwa mwezi na anapotolewa saloni huvalishwa vitu miguuni na kwenye mkia ili kumzua asichafuke pindi anapotembea.
2. Rangi anayopenda sana ni Pinki, hii ni kutokana gauni lake la awali kuvalishwa lilikuwa na rangi hiyo, hivyo imemkaa sana kichwani mwake, pia hupenda kuvalia tai Nyekundu.
3. Kuna muda humsindikiza Wema kwenda kushuti filamu, akiwa huko hupenda kusikiliza muziki na kula karanga wakati akimsubiri Bosi wake huyo warudi wote nyumbani.
4. Chakula chake kikubwa ni nyama ambayo tayari imepikwa ingawa anaweza kula mbichi kama mbwa wengine, na hupendelea kunywa Mvinyo baada ya kula. 5. Anapopanda gari na Wema hupendelea kuketi siti ya mbele, na mara kadhaa amekuwa akijaribu kutaka kuendesha ingawa hajawahi kupewa fursa hiyo. 6. Ana ukurasa wake wa Instagram ambapo anafuatiliwa (followers) na watu zaidi ya 23.9k. Watu wengi huonyesha kuvutiwa na mtindo wake maisha.
7. Wema anadai huyu ni sawa na mtoto wake na anampenda sana. “Ndiyo, ananipenda sana, sio kwa sababu ni Mbwa bali kama mtoto wake,” inasema moja ya taarifa kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa Manunu.
8. Kuna wakati hupewa fedha kwa ajili ya matumizi yake ya wikiendi tu, na hizo sio chini ya Sh20,000. Hivyo ni yeye kuamua kama ataenda kununua nyama choma au Mvinyo.
9. Ana kitanda chake maalum cha kulalia alichonunuliwa kutoka duka la Pillow Lady, na baada ya kula mchana hupenda kulala walau saa mbili kisha kuendelea na mambo yake.
10. Yote uliyosoma ni machache ya yale anayofanyiwa Mbwa huyu, Wema anasema anafanya hivi kwa upendo tu na wale wanamkosoa kwa kusema bora angefanya hivyo kwa watoto wenye uhitaji, wafahamu kuwa sadaka amekuwa akitoa kila wakati ambazo huwenda kufanya hivyo pia.