Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"Mama yangu hayupo sawa hadi leo" - Meja Kunta

Wed, 13 May 2020 Chanzo: --

Msanii wa Singeli Meja Kunta, amefunguka na kusema kashfa na kiki zilizotokea zimemsababishia mama yake mzazi kutokuwa sawa kiafya.

Akizungumza na eNewz ya East Africa TV, kuhusu kashfa na kiki zinazomtokea Meja Kunta amesema , "Kwa upande wangu hata mimi sizipendi, kitu ambacho ningeweza kufanya labda ni kuitisha watu au vyombo vya habari na nikaliongelea lile suala ili kujitoa na jinsi gani ya kujisafisha ili nisionekane mbaya".

"Kilichofanyika kimemuumiza sana Meja na kimemsababishia matatizo hadi kwa Mama yangu mzazi kwa sababu, hadi leo hii hayupo sawa amekuwa ni mtu wa kuanguka kiufupi hayupo sawa, kitu ambacho kinanipa mawazo sana kwa sababu sikuwahi kufirikia hata siku moja kama naweza kusababisha matatizo" ameongeza.

Chanzo: --