NI Headlines za mzazi mwenza na staa wa Bongo Fleva Harmonize aitwae Shantee ameibuka baada ya kuona mwanae kabebwa na Mwigizaji wa Filamu Kajala akiwa na Harmonize visiwani Zanzibar.
Mzazi mwenza wa Harmonize kayaandika haya…’Baba Zuu nakuja huku unapopenda wewe ninachoomba huyo mtoto harudi nyumbani tafadhali labda nikuulize, Baba gani anaweza mchukua mtoto bila ya kuwasiliana na mzazi mwenzie?, sababu unanidharau si ndio? ‘– Mzazi mwenza na Harmonize
‘Baba gani anaweza mchukua mtoto kwenda sehemu ya mbali bila dada wa mtoto?anaishije, anakula nini? niliongea na wewe sana mlivyoenda mwanza lakini nahisi huna uchungu na mtoto kabisa’– Mzazi mwenza na Harmonize