Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama wa Sean Kingston atoka Gerezani

Sean Kingston Mama Mama wa Sean Kingston atoka Gerezani

Thu, 30 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama wa mwimbaji Sean Kingston “Janice Turner” ameachiliwa kutoka kwenye mikono ya polisi baada ya kukaa kwa siku nne gerezani, Mama huyo ameachiliwa Jumatatu Mei 27, baada ya kukamatwa wakati wa uvamizi katika nyumba ya mtoto wake iliopo Florida, ambapo polisi alimuweka chini ya ulinzi kwa madai ya ulaghai na wizi.

Kama ilivyoripotiwa hapo awali Janice Turner (Mama wa Kingston) mwenye umri wa miaka 61, aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi kwa tuhuma ya ulaghai na wizi wakati wa uvamizi, rekodi za mahakama zinaonyesha kwamba anakabiliwa na mashtaka manane, ikiwa ni pamoja na kuendesha njama iliyopangwa ya ulaghai, wizi mkubwa na wizi wa utambulisho

Turner ametolewa nje kwa dhamana ya Dollar 160,000 sawa na Tsh Millioni 416.8

Chanzo: www.tanzaniaweb.live