Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama wa Notorious atangaza kumchapa Vibao P. Diddy

Voletta Wallace And Diddy Mama wa Notorious atangaza kumchapa Vibao P. Diddy

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama mzazi wa marehemu Notorious B.I.G “Violetta Wallace” amefunguka ya kuwa siku akikutana na rapa Diddy, atampiga kibao mchana kweupe.

Mama Violetta ametoa kauli hiyo mara baada ya kufanya mahojiano na jarida la Rolling Stone, chapisho la alhamis Mei 30, 2024. Kauli hiyo imekuja kutokana na kuona video inayomuonesha Diddy akimfanyia unyanyasaji aliyekuwa mpenzi wake Cassie tukio lililotokea mwaka 2016.

Mama Violetta amesema “Natumai kuwa nitamuona Sean siku moja na kitu pekee ninachotaka kufanya ni kumpiga kibao mchana kweupe” pia amesema ya kuwa yupo pamoja na Cassie na anafanya maombi kwa Mungu kwa ajili yake na mama yake.

Rapa Diddy alikuwa na ukaribu na Mama yake Notorious kupitia mwanaye ambaye alikuwa msanii wake kupitia lebo ya ‘Bad Boy Records’ na Notorious alifariki dunia mwaka March 9, 1997.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live