Mama wa aliyekuwa mwanamuziki kutoka nchini Afrika Kusini, marehemu Costa Titch ametoa malalamiko kwa Maabara ya Afya ya Taifa nchini humo kushindwa kutoa matokeo ya kipimo cha marehemu mwanae kwa haraka.
Ameomba msaada wa haraka kupata majibu ya kipimo cha mwanae na kudai kuwa kutokana na kutokuwepo kwa majibu hayo kunapelekea polisi kushindwa kufanya lolote kuhusiana na kifo cha mwanae.
Mama huyo ameandika hayo kupitia ukurasa wa instagram wa Costa Titch ambao mwezi mmoja baada ya kifo cha mwanae alianza kuendesha ukurasa huo. Nyota huyo wa Afrika Kusini alifariki mwezi Machi alipokuwa akitumbuiza jukwaani.