Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Mama mzazi wa Jay Z afunga ndoa na mwanamke

Gloria Carter Roxanne Wiltshire Mama mzazi wa Jay Z afunga ndoa na mwanamke

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwaka 2017 rapa Jay Z kupitia wimbo wake 'Smile' alifunguka namna ambayo mama yake mzazi anavutiwa na mapenzi ya jinsia moja.

"Mama alikuwa na watoto wanne, lakini yeye ni msagaji/ilimbidi ajifanye kwa muda mrefu kiasi kwamba yeye ni thespian/ilibidi ajifiche chumbani, hivyo alitibu/aibu ya jamii na maumivu yalikuwa mengi mno," alisema mshindi huyo wa Grammy mwenye umri wa miaka 53 katika wimbo huo.

"Machozi ya kilio cha furaha ulipoanguka kwa upendo / haijalishi kwangu ikiwa ni yeye au ninataka tu kukuona ukitabasamu kupitia chuki/Marie Antoinette, mtoto, wacha tule keki..." alisema Jay Z.

Sambamba na hilo, mama mzazi wa Jay Z (Gloria Carter) amemuoa mchumba wake wa muda mrefu, Roxanne Wiltshire.

Harusi hiyo imefanyika Marekani, imehudhuriwa na watu mashuhuri kama Beyonce, Jay-Z, Kelly Rowland, Robin Roberts, Tyler Perry, Tina Knowles-Lawson, na wengine.

Mama mzazi wa Jay Z alianza uhusiano na Roxanne mwaka 2018, wamefanikiwa kufunga ndoa tarehe 2 Julai, 2023, jambo ambalo katika maadili ya nchi za bara la Afrika halikubaliki na linapigwa vita kubwa.

Roxanne ni mtoa misaada/mfadhili, mwanzilishi mwenza na Rais wa Roxanne Foundation.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live