Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama Tetema ya Rayvanny Ft. Maluma yafutwa YouTube

Billboard RAYVANNY MALUMA Mama Tetema ya Rayvanny Ft. Maluma yafutwa YouTube

Wed, 24 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni wiki kadhaa tangu video ya wimbo wa msanii Rayvanny aliyomshirikisha bosi wake, Diamond Platnumz uitwao ‘Tetema’ kufutwa kwenye mtandao wa YouTube, kisha kurudishwa tena siku nne zilizopita, sasa ni zamu ya ‘Mama Tetema’.

Producer wa biti ya wimbo huo, Salimin Kassim ‘S2Kizzy’ ambaye alidaiwa kuiondoa ‘Tetema’, sasa anadaiwa tena kuhusika kuifuta video ya ‘Mama Tetema’ katika mtandao huo wa YouTube, wimbo ambao rayvanny alifanya na msanii mkubwa kimataifa, Maluma.

Mama Tetema iliachiwa hewa katika mtandao wa YouTube mnamo Novemba 2021, na sasa haipo hewani tena.

Katika video ya wali, S2Kizzy alikana kuhusika kuifuta video hiyo huku wadukuzi wa mambo wakidai kuwa producer huyo ndiye aliyehusika kwani jina linaonekana ni la kwake lililoifuta na kisa ni kwamba anamdai Rayvanny mkwanja mrefu wa kuandaa audio ya wimbo huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live