Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama Raya awaka: Barnaba hana adabu

Mama Kimbo Barnaba Mama Raya awaka: Barnaba hana adabu

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama mkwe wa msanii wa Bongo Fleva Barnaba aitwaye Mamakimbo amegeuka Mbogo kwa mkwewe baada ya picha na video za location alizoshare Barnaba kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa na msanii Yammy ambapo amesema zimesababisha mwanae Raya the Boss arudi nyumbani.

“Barnaba hana adabu, anamchezea mtoto wangu, nimeshazungumza naye na nitazungumza naye tena, mshenga wake nitazungumza naye na mwanangu nitamchukua. Huwezi kwenda kumshika mwanamke kiuno ch**pi imepanda mpaka juu wakati umeoa ni mume wa mtu, ni nidhamu hiyo kweli? Ni kazi gani hiyo? Unatakiwa ujiheshimu uwe mstaarabu ujipende, mambo ya ajabu mimi sijapenda kabisa.

“Ukiwa mume wa mtu unatakiwa kuwa na mipaka sio kila mwanamke unamshika shika tu, unamdhariridha mtoto wangu. Huwezi kushikwa namna ile hata kama unaigiza kama mke wa mtu nitavaa vizuri nitaigiza kwa stara zangu nzuri, nitashikwa kidogo ila sio vile.

“Yammi ajiheshimu akae kwa kutulia na ajue Barnaba ni mume wa mtu na akifanya kazi na Barnaba awe na utuo. Barnaba namwambia tafahdari umemuoa mwanangu kaa kwa kutulia uwe na adabu na heshima, uangalie wanawake wa kupiga nao picha sio kupiga picha hovyo hovyo. Barnaba tulikuwa tunapatana lakini tangu picha hizi zimetoka tumeshatibuana tena na sitaki kabisa kumuona.

“Video gani ile wamepiga? Sasa hivi kuna ugomvi kati ya Barnaba na Raya na sasa hivi Raya yupo nyumbani kwangu ameshaondoka nyumbani kwake na mpaka tuzungumze na Barnaba na mshenga wake ndiyo atarudi nyumbani kwake. Barnaba kama anataka kumuongeza Yammi kama mke wa pili anaruhusiwa amuongeze tu tujue kama Raya ana mke mwenza lakini sio kushikana namna mingine.

“Barnaba aje kwangu na mshenga wake, aombe radhi kwa mkewe mbele yangu halafu zile picha zote azifute zisiwepo,” amesema Mama Kimbo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live