Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama Diamond akanusha penzi la mwanaye na Zuchu 'sio wapenzi'

Mama Diamond Akanusha Penzi La Mwanaye Na Zuchu 'sio Wapenzi'.png Mama Diamond akanusha penzi la mwanaye na Zuchu 'sio wapenzi'

Wed, 3 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama Dangote kwa mara ya kwanza amezungumzia ukweli uliopo kwa kile ambacho kwa zaidi ya mwaka mmoja kimekuwa kikitajwa kuwa mwanawe Diamond anatoka kimapenzi na Zuchu.

Mama Dangote alilazimika kunyoosha maelezo kuhusu sekeseke hizi ambazo zimekolezwa munyu kwa zaidi ya mwaka mmoja kuhusu uhusiano wa Zuchu na bosi wake, baada ya Diamond kuonekana akiigiza kama mbeba maudhui mkuu kwenye video ya wimbo mpya wa Zuchu, Utaniua.

Hii ndio mara ya kwanza kwa Diamond kuigiza kwenye video ya wimbo ambao hajashirikishwa na baadhi ya maudhui kwenye wimbo huo ni ya kimapenzi ambayo Diamond aliigiza barabara kama mhibu wa Zuchu.

Matukio hayo kwa mara nyingine yaliotesha uvumi wa wawili hao kuwa katika mapenzi kwani njia ambazo wanakumbatiana katika sehemu moja wakiwa wamelowa kwa kunyeshewa inaashiria mahaba na upendo wa kweli.

Lakini Mama Dangote alikanusha vikali hilo pia akisisitiza kwamba mwanawe Diamond hajawahi kuwa katika uhusiano wa mapenzi na Zuchu bali ni biashara tu na ili kunogesha biashara ya kimuziki, ilibidi ‘wachangamshe genge’ kwa kuigiza huba.

“Hakukuwa na mahusiano. Tulikuwa tunachangamsha genge tu ili tutrend,” Mama Dangote alisema.

Miezi michache iliyopita, baada ya kushindwa tena kuendelea na wimbi la kuhusishwa kimapenzi, Zuchu akiweka taarifa kwamba uhusiano wake na Diamond umekwisha na kutangaza kuwa singo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live