Mama mzazi wa mwanamuziki Diamond Platnumz, Bi Sandrah maarufu Mama Dangote, amempongeza kijana wake huyo kwa kununua ndege yake binafsi (Private Jet).
Mama Dangote ambaye hivi karibuni alisherehekea kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa, ametumia insta story yake kutoa pongezi hizo pamoja na kumshukuru Mungu kwa jambo hilo kubwa alililolifanya mwanaye.
"Allhamdulilaah, Mungu mkubwa leo hii unamiliki ndege Naseeb @diamondplatnumz," ameandika Mama Dangote.
Ikumbukwe, Diamond kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni na DW nchini Ujerumani, amethibitisha kuwa amekwisha nunua ndege yake hiyo binafsi.
Pia, katika mahojiano yake mengine aliyoyafanya nchini Ivory Coast miezi miwili iliyopita, Diamond alisema ndege hiyo itatua nchini kabla ya mwezi Oktoba.