Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mama Dangote adaiwa kumpiga chini Anko Shamte

MAMA DANGOTE ANKO SHAMTE Mama Dangote adaiwa kumpiga chini Anko Shamte

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mama mzazi wa supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, Mama Dangote na mumewe Uncle Shamte wanadaiwa kutengana.

Wawili hao wameacha kufuatiliana kwenye mitandao ya kijamii na kuzua tetesi kuwa ndoa yao inaweza kuwa ikipitia changamoto.

Uncle Shamte naye hivi karibuni alilenga maswali ya mashabiki mitandaoni baada yake kukosa kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa mpenziwe, Mama Dangote.

Tofauti na hapo awali, wanandoa hawa wameacha kuchapisha picha zao wakiwa pamoja kama ilivyokuwa hapo awali na Uncle Shamte amepuuza maswali ya mashabiki kuhusu hali ya ndoa yao.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kwa nini hivi karibuni aliblockiwa na Mama Diamond baada ya miaka mitano kwenye ndoa, Shamte alisema;

"Hilo ni jambo la kawaida. Haya mambo yanatokea, yeye ni binadamu na mimi ni binadamu. Hatujakuwa tukipostiana kwa muda mrefu zaidi. Mitandao ya kijamii ni jambo lisilo na maana na sisi sote tuna biashara pamoja ambayo tunashughulikia."

“Nifuate tu kwenye mitandao ya kijamii, nitakuambia ukweli,” aliongeza.

"Sisi ni watu wazima. Hatuna tofauti. Tofauti za nini?"

Baadhi ya wanamitandao waliibua hisia mseto kutokana na hilo na kusema;

Chidi Boyi: Mama dangote kazaliwa vipi mkuu sio kawaida yako

Salum156: Mbona hujamuwish mama dangote birthday

umaedith: washaachana kitambo, mopao kachukua nafasi

EstherMgonya: asi nilitaka kuuliza maswali Ila majibu nimeyapata kwenye Comment, Vina Mudaaaaaa

Bibiyakempenzi: Maadogo yana wenyewe, yani mliachana yani mkaanifolliana

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: