Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maluma apagawa na "tetema" ya Rayvanny ft. Diamond

Maluma 660x400.jpeg Maluma apagawa na "tetema" ya Rayvanny ft. Diamond

Sun, 18 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Tunaweza kusema wiki hii imekua wiki nzuri kwa Sanaa ya Tanzania ambapo baada ya Mwigizaji Idris Sultan kututangazia habari kubwa ya kuanza kuonekana Netflix, Mwimbaji Staa Mzaliwa wa Colombia Juan Luis Arias maarufu Maluma amedata na ‘tetema’ ya Rayvanny ft. Diamond Platnumz.

Maluma ambae ana follower milioni 57 Instagram, ameonekana kwenye video na Marafiki zake wakiifurahia ‘tetema’ ambayo ni smash hit iliyoachiwa February mwaka 2019 na hadi sasa ina views milioni 55 Youtube, C.E.O wa Next Level Music Rayvanny amethibitisha uwezekano wa wawili hao kufanya remix ya ‘tetema’ lakini pia kufanya ngoma yao nyingine nje ya hiyo remix.

“Sasa haitokua remix tu kuna ngoma lingine pia, acha tuone… Big thanks to my Brother @maluma tetema vibe this is next level iiiish” ——— aliandika Rayvanny.

Maluma ni miongoni mwa Super Stars wa dunia wenye rekodi za kufikisha views bilioni moja youtube kwa wimbo zaidi ya mmoja ambapo smash hit yake ya ‘Felices los 4’ ina views 1.6 billion huku ‘corazon’ ikiwa na 1.5 Billion kwenye youtube yake yenye Subscribers milioni 27. 

https://www.instagram.com/p/CNy1K7JDIZU/?utm_source=ig_web_copy_link

Chanzo: millardayo.com