Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malkia Karen mtoto wake ‘hana baba’ nilichukua mbegu nikaweka kwangu

Malkia Karen Ml Malkia Karen na mtoto wake

Tue, 5 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Bongo Fleva, Malkia Karen ameianika sura ya mtoto wake kwa mara ya kwanza tangu alipojifungua mnamo mwezi Novemba mwaka jana 2021.

Kareen ambaye ni mtoto wa mtangazaji nguli wa radio, Gardiner G Habash amesema watu wengi wamekuwa wakimuuliza kuhusu baba wa mtoto huyo ambaye hajawahi kumtaja popote huku akieleza kwamba yeye alipandikiza mbegu na kupata mtoto badala ya kulala na mwanaume.

“Siku hizi ukitaka mtoto sio lazima mfanye physical contact, kila siku naulizwa baba mtoto yupo wapi issue ni kwamba nilipofikia uamuzi wa kupata mtoto, sikuweza kupata mwenza wa kupata naye mtoto.

“Nilichokifanya nilienda hospitali nikachukua mbegu za kiume nikaziweka kwangu ni suala la dakika tano tu. Hicho ndo nilichokifanya, hiyo issue ilinitesa sana, kuna mbegu ambazo zipo donated hospitalini,” amesema Malkia Karen.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live