Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malkia Karen ataja sifa za mwanaume anayemhitaji

94771 Karen+pic Malkia Karen ataja sifa za mwanaume anayemhitaji

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Karen Gardner, mtoto wa mtangazaji maarufu nchini Tanzania, Gardner Habash ametaja sifa za mwanaume anayemhitaji.

“Napenda mwanaume mwenye hofu ya Mungu, anayeweza kunisaidia na kuipenda familia,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Februari 6, 2020 katika mahojiano na MCL Digital ikiwa zimepita siku kadhaa tangu baba yake kueleza kuwa anatamani mwanaye awe na uhusiano na mwanaume aliyemzidi umri ili aweze kumlea.

Alipoulizwa kuhusu kauli ya baba yake, Karen amesema watu walimuelewa vibaya kwa maelezo kuwa Gardner ambaye ni mtangazaji wa Redio Clouds alitamani kuona akiwa na mwanaume wa aina fulani, si kwamba anampangia.

“Hizo ndio sifa za mtu ninayemtaka, kuhusu umri, kimo na rangi hayo siwezi kuyasema kwani bado sijakutana naye na kama mnavyojua  mapenzi  hayaangalii hayo unaweza kusema unamtaka mweupe akaja mweusi na ukajikuta unampenda.”

“Ukisema sema unamtaka mwenye umri  mkubwa akaja kijana, na ndio maana unaweza kumpenda mtu lakini jamii ikakunyooshea kidole kuwa umempendea nini,” amesema Karen.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz