Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mali za Tekashi kupigwa mnada kulipa fidia

Tekashi6ix9ine Mali Mali za Tekashi kupigwa mnada kulipa fidia

Mon, 18 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rapa kutoka nchini Marekani, Tekashi6ix9ine atalazimika kuuza mali zake za thamani ili kulipa faini ya dola 9.8 milioni, ambazo ni zaidi ya tsh 24 bilioni, kufuatia uamuzi wa jaji wa Florida katika kesi ya kumpiga kichwani na chupa Alexis Salaberrios katika klabu ya ‘strip’ mwaka 2021.

Jaji Robert T. Watson amethibitisha uamuzi huo kwa rapa huyo baada ya kushindwa kufika Mahakamani kupinga uamuzi huo mwezi Julai mwaka huu.

Mali zinazotakiwa kuuzwa ni pamoja na gari aina ya Rolls-Royce, jumba lake la kifahari la Florida na vitu vingine vya bei ghali ambavyo vinaweza kuuzwa kwa mnada ili kulipa fidia ya dola milioni 9.825.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live