Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Malezi mabovu chanzo cha kuporomoka maadili-Waziri Gwajima

Waziri Gwajima Azindua Mradi Wa Kuimarisha Afya Vijana Wa Mazingira Hatarishi Malezi mabovu chanzo cha kuporomoka maadili-Waziri Gwajima

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa kulegea kwa malezi na makuzi kwa ngazi ya familia ni chanzo kikubwa cha kuporomoka kwa maadili kwa watoto na vijana rika.

Akizungumza hayo jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na Viongozi wa dini juu ya uzinduzi wa Tamasha la Maendeleo, alisema moja ya agenda katika taifa ya hivi sasa ni changamoto ya mmomonyoko wa maadili ambayo inachochea kwa kiasi kikubwa kuibuka kwa ukatili wa kijinsia kwa watoto.

Alisema jamii inapaswa kutazama ukubwa wa tatizo hili kwa sasa na kuona ni namna gani watoto na vijana walivyoporomoka kimaadili na kuchukua kama changamoto ambayo wataweza kukabiliana nayo na kuweza kuifanyia kazi katika kuwafundisha maadili mazuri.

Dkt.Gwajima alisema ili tatizo hili liweze kutatulika ni ushirikiano baina ya Serikali na jamii ambapo kila mtu anapaswa kujia wajibu wake katika kuhakikisha vijana na watoto wanaangaliwa tangu wakiwa na miaka 0 hadi 18.

Aliwaomba viongozi wa dini kusimamia agenda zinazoruhusu maendeleo na ustawi wa jamii hususani malezi na makuzi ya kiroho na kukemea ukatili wa kijinsia kwa watoto katika maeneo ya nyumba za ibada.

Akizungumzia tamasha la Maendeleo, Dkt. Gwajima alisema serikali, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, wameandaa tamasha hilo linatarajiwa kuzinduliwa Viwanja vya Leaders Klabu Aprili 27 hadi 29, 2023 lenye lengo la kuhamasisha jamii kuzijua fursa za kiuchumi sambamba na kukemea ukatili wa kijinsia na watoto.

Kwa Upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Dar es Salaam, Nyamala Elisha alisema tatizo la mmomonyoko wa maadili nchini umekuwa mkubwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo malezi pamoja na migogoro ndani ya ndani.

Alisema sababu hizo zimekuwa ni changamoto kubwa kusababisha mmomonyoko wa maadili kwa sasa kushika kasi hivyo ni wajibu wa taifa kwa ujumla kuungana na kuhakikisha maadili ya watoto yanarudi kama miaka ya nyuma licha ya uwepo wa undawazi kukua dunia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live