Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Malcolm X aliuawa siku kama ya leo

Malcolm Little X Malcolm X.

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanaharakati wa haki za watu weusi Malcolm Little ama el-Hajj Malik el-Shabazz maarufu kama Malcolm X aliuawa tarehe 21 Februari, mwaka 1965 .

Malcolm X alizaliwa Mei 19 1925 Omaha, Nebraska, Marekani. Jina lake halisi lilikuwa "Malcolm Little" lakini aliamua kubadili jina na kujiita Malcolm X ambapo X ina maana ya kitu kisichojulikana. Alitumia X kuficha jina lake la ukoo ili ukoo wake wa kiafrika usijulikane.

Kipindi cha ujana wake alijikita kwenye wizi na ujambazi hali hii ilipelekea akamatwe ahukumiwe kwenda jela. Kipindi yupo jela alikutana na moja ya viongozi wa chama cha waislamu "Nation of Islam" aitwaye "Eliyah-Mohamed".

Baada ya muda wa kifungo cha Malcolm X kuisha alitoka jela na alikuwa bado Mkristo, akawa anaenda kwenye makanisa ya wazungu lakini akaona mafundisho yao ni kama ya kuwafanya waafrika kuendelea kuwasujudu na kuwanyenyekea wazungu kwa kila jambo.

Baada ya hapo akaenda Macca ambapo akaslimu rasmi na kuacha jina la Malcolm X na kujiita EL-HAJJI MALIK EL SHEBAAZ. Malcolm X akiwa Mwanachama wa Chama cha waislamu wanaopambania haki za Waafrika "Nation of Islam" alikuwa ana ushawishi mkubwa pamoja na misimamo ambayo baadhi ya watu waliogopa kufanya naye kazi kwa kuogopa nafasi yao kuchukuliwa na yeye.

Mwanzoni mwa miaka ya 1960s misuguano kati ya yeye na viongozi wa Chama hiki ilizidi, hivyo akaamua kujitoa na akaanzisha "Islamic Muslim Mosque, Inc. (MMI)" na "Pan-African Organization of Afro-American Unity (OAAU)" baada ya kuanzisha taasisi zake ugomvi na Chama alichokuwa zamani ulikua zaidi maana mara nyingi walikuwa wakipingana kwa hoja kwenye mihadhara na mikutano mbalimbali.

Baada ya hapo alianza kupokea vitisho vya kuuawa na Mwaka 1965 ndipo aliuawa kwa risasi Jijini Newyork akiwa na umri wa miaka 39. Baada ya mauaji hayo vijana kadhaa kutoka Kundi la "Nation of Islam" walikamatwa kwa madai ya kumuua Malcolm X.

R.I.P Malcolm X.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live