Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Malaysia yasitisha tamasha baada ya wanaume wawili kubusu jukwaani

Malaysia Yasitisha Tamasha Baada Ya Wanaume Wawili Kubusu Jukwaani Malaysia yasitisha tamasha baada ya wanaume wawili kubusu jukwaani

Sat, 22 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Malaysia imesitisha tamasha la muziki katika mji mkuu Kuala Lumpur siku ya Jumamosi, siku moja baada ya mwimbaji wa bendi ya muziki ya pop ya Uingereza The 1975 kumbusu mwanamuziki mwenzake wa kiume jukwaani na kukosoa sheria za nchi hiyo dhidi ya kundi la wapenzi wa jinsia moja (LGBT).

"Hakutakuwa na maelewano dhidi ya chama chochote kinachopinga, kudharau na kukiuka sheria za Malaysia," Waziri wa Mawasiliano Fahmi Fadzil alisema katika chapisho la Twitter.

Kundi la The 1975 pia wamepigwa marufuku kutumbuiza nchini Malaysia, ilisema kamati ya serikali ambayo inasimamia filamu na maonyesho ya wageni.

Mpenzi ya jinsia moja ni uhalifu katika nchi ya Malaysia yenye Waislamu wengi.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yameonya juu ya kuongezeka kwa kutovumilia dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na wale waliobadili jinsia.

Katika video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii Ijumaa jioni, Healy alionekana akimbusu mpiga besi Ross MacDonald baada ya kukosoa msimamo wa Malaysia dhidi ya LGBT katika hotuba iliyojaa lugha chafu kwa hadhira ya tamasha.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live