Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makubwa! Paula anawafokea wateja wake huko

Paula Awafokea Makubwa! Paula anawafokea wateja wake huko

Sat, 20 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paula Kajala; ni mrembo maarufu nchini Tanzania ambaye anadaiwa kuwafokea baadhi ya wateja wake wanaodai anauza nguo zake bei ghali katika duka lake alilofungua hivi karibuni.

Baadhi ya wateja wanalalamika kwamba, kwenye duka hilo nguo ya bei ya chini ni shilingi elfu sabini na tano huku miwani akiuza shilingi elfu hamsini huku mtu akijaribisha zaidi ya mara mbili, basi Paula anadaiwa kukasirika na kufoka.

Hata hivyo, baada ya malalamiko hayo, Paula ameibuka na kuwachana wateja hao kwa kusema;

“Hebu kuweni serious nyie, yaani vitu vya Zara au H&M niwauzie elfu 20? Hamko serious, mnasikitisha…”

Paula alisema duka hilo limemgharimu shilingi milioni 500 za Kitanzania, jambo ambalo limepingwa na wengi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live