Dunia ina mambo hii nyie acheni! Msanii kutoka Zanzibar Smile ametamba kuwa yeye pamoja na wasanii wenzake wanaotokea visiwani Zanzibara wana uwezo mkubwa wa kuimba kuliko wasanii wengi wa bara hususan Dar es Salaam.
Amesema, wasanii wengi wa Dar wanapenda tu sifa zisizo na maana kuringishia hata vitu ambavyo hawana katika uhalisia.
“Mimi ni msanii mkubwa, nina hela na sio za leo. Eti kuna msanii niliona eti anaringia Crown wakati hilo mimi nilikuwa nalo kama miaka mitatu iliyopita,” alisema.
Msanii huyo amesema anatamani kuwepo hata na mpambano wa wasanii wa Zanzibar na wa Bara ili waweze kuthibitisha ubora wa wasanii kutoka Zanzibar.