Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Makonda: Chukueni vyote ila mniachie Maria wangu

Makonda Tuh Makonda na mkewe.

Fri, 3 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Christian Makonda amemwagia sifa kedekede mkewe, Maria ikiwa jana ni kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya mwanamama huyo.

Makonda kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika maneno haya kwa mkewe;

"Dunia imebeba mengi sana ila mimi nimekubali kubebwa nawe kipenzi changu, kwani wewe ndiye Dunia yangu, chochote wachukue lakini waniachie wewe, Maria wangu, mwanamke wa maisha yangu, NAKUPENDA MNOO!!

"Ninaamini MUNGU hutubariki, lakini Baraka zake hupitia kwa watu, wewe ndio yule mtu, uliebeba za kwangu, ambae kupitia wewe naona vingi maishani mwangu, nataka nikwambie jambo moja, unapendwa mnoo na Makonda.

"Popote unapopita ringa na tembea kifua mbele ukiamini hakuna mwanaume anaekupenda kama mimi, kwako hata ashushwe mwanamke wa namna gani na asemwe kwa sifa zote za uzuri bado nakiri hakufikii.

"Kwako sioni sisikii, nakupenda mnoo, na katika siku yako hii kubwa nataka nikwambie MOYO wangu unao wewe, Happy Birthday kipenzi changu, Mama wa watoto wangu, nakuombea umri mrefu ili niendelee kufaidi Nuru ya uzuri wako kwenye himaya yangu, hapa ni KUFA na Kuzikana!! Happy Birthday my love!!," amesema Makonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live