Menu ›
Burudani
Wed, 12 Oct 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Msanii memba wa Makomando, Muki amefunguka kuewa kundi lao la muziki halijafa isipokuwa wameliweka pembeni kwa muda.
Akizungumza na kipindi cha Refresh cha Wasafi TV, Muki alisema, yeye na Fred wamejipa nafasi kila mtu afanye ngoma kama msanii solo lakini baadaye itakapotokea wamepata mzuka wa pamoja, watafanya kama kundi.
“Tumefanya maamuzi haya sababu ya kila mtu kupata nafasi ya kuwaza na kufanya ngoma maana unaweza ukawaza kumbe mwenzako wakati huo hana mzuka hivyo tumejipa nafasi lakini kundi lipo na kuna wakati tutafanya kama kundi,” alisema Muki.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live