Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makala: Khaligraph Jones anatuma ujumbe gani katika Bongo Flava?

Mon, 29 Jan 2018 Chanzo: bongo5.com

Kwa sasa ukipanga Playlist ya ngoma za hip hop kutoka Afrika Mashariki ikakosekana ngoma ya Rapper Khaligraph Jones kutoka nchini Kenya itakuwa ni kuukosea heshima muziki huo.



Khaligraph Jones anasifika kuwa na uwezo mkubwa wa free style na kupanga punch line katika ngoma zake, pia ana uwezo mzuri katika kutumia lugha ya Kiswahili na kingereza.

Khaligraph Jones na Bongo Flava

Kutokana na uwezo wake ameweza kufanya kolabo na wasanii kadhaa kutoka Bongo na ngoma hizo kufanya vizuri.

Kwa mara kwanza kumsikia Khaligraph katika ngoma moja na msanii kutoka Bongo ni pale alipomshirikisha Nikki Mbishi katika ngoma yake inayokwenda kwa jina Baba Yao.

Baada ya ngoma hiyo na Nikki Mbishi alikaa muda kidogo bila kusikika katika kolabo na msanii wa Bongo ila alipokuja kurudi ndio inapelekea kuandika makala haya.

Rosa Ree

Rapper huyo ambaye ametamba na ngoma kama Up in the Air, Dow na nyinginezo aliweza kufanya kolabo na Khaligharaph Jones kupitia ngoma yake ya One Time ambayo waliifanyia remix.

Wakati remix hii inatoka Rosa Ree bado alikuwa chini ya usimamizi wa label ya The Industry.

Kutokana na aina ya rap anayofanya Rosa Ree kukutana na Khaligraph katika ngoma moja vilikutana vitu viwili ambavyo vina uwiyano sawa.

Remix hii ambayo ilitoka June mwaka jana ndio ilikuwa ngoma ya kwanza kwa Rosa Ree kumshirikisha msanii mwingine na toka hapo hajafanya hivyo zaidi ya yeye kushirikishwa.

Young Killer

Kolabo kati ya Young Killer na Khaligraph Jones ni moja ya project ambazo zilikuwa zikisubiriwa kwa muda Bongo na mashabiki ili imekuja kutoka bila kuwa na uzito wake ambao ulikuwa ukitariwa.

Sababu ni kwamba ngoma hiyo ‘Shots’ ilivuja mtandaoni kabla ya Young Killer kuitoa rasmi ikiwa imekamilika hivi karibuni (January 24).

Chin Bees

Chin Bees amlishirikisha Khaligraph Jones katika remix ya ngoma ‘Kababaye’, hii ilikuwa ni remix ya pili kwa Khaligraph kufanya na msanii kutoka Bongo.

Khaligraph aliweza kuonyesha uwezo mkubwa katika kupitia juu ya mdondo wa trap wa ngoma hiyo ambao ulifanyika Wanene Entertainment na producer Luffa.

Remix ya Kababaye ambayo ilitoka October mwaka jana iliambatana na remix ya ngoma ‘Nyonga Nyanga’ ambayo alimshirikisha Wyre na Nazizi wote kutoka nchini Kenya ila ile ya Khaligraph Jones ilikuwa na nguvu zaidi.

Christian Bella

Huyo ndiye msanii wa kwanza kwa mwaka jana kuachia ngoma na Khaligraph Jones, walitoa wimbo uitwao Ollah ambao ulitoka mwishoni  mwa January.

Pia ndiye msanii wa kwanza ambaye anaimba kufanya hivyo, wote niliowataja kasoro Rayvanny ambaye anarap na kuimba, wanafanya muziki wa rap.

Christiana Bella amekuwa akishirikishwa na wasanii kadhaa wanaofanya muziki wa rap/hip hop kwa hapa Bongo, alishawahi kufanya chorus ya ngoma ya Fid Q ‘Roho’ na ile ya Weusi ‘Nijue’.

Hata hivyo alipotaka michano katika ngoma yake ilimbidi kuvuka boda hadi Kenya kuinasa sauti ya Khalighraph Jones.

 Stereo  

Baada ya kufanya vizuri na ngoma ‘Mpe Habari’ ambayo alimshirikisha Rich Mavoko aliona kuna umuhimu wa ngoma hiyo kuwa na remix.

Stereo aliweza kuwakutanisha wasanii kutoka Bongo na nje katika remix aliyofanya, kutoka Bongo walioshiriki ni Bill Nass, Stamina na Jay Moe huku kutoka nje akiwa ni Khaligraph Jones.

Hii ilikuwa ni ngoma ya tatu kwa Khaligraph kushiriki remix yake baada ya One Time ya Rosa Ree na Kababaye ya Chin Bees, Mpe Harari remix ilitoka October mwaka jana.

Rayvanny

Licha ya Rayvanny kufanya vizuri katika muziki wa kuimba pia ni mzuri sana katika rap.

Hii inapelekea kumuana katika ngoma kadhaa za hip hop, mwaka jana alishirikishwa na Fid Q katika ngoma remix ya ngoma ‘Fresh’, kabla ya hapo alikuwa amesharudia ngoma ya Mr. II ‘Sugu’.

Hivyo basi haikuwa ni mshangao pale walikutana studio na Khaligraph Jones na kutoa ngoma ‘Chalii ya Ghetto’, ngoma hii ilitoka May mwaka jana.

Hitimisho

Ukifuatilia kwa karibu utagundua kipindi cha takribani mwaka mmoja Khaligraph Jones ameshirikiana na wasanii wengi sana wa Bongo.

Kuanzia January mwaka jana aliposhirikishwa na Christian Bella katika wimbo ‘Ollah’ hadi January mwaka huu ambapo ameshirikishwa na Young Killer, kwa kipindi hicho amefanya kolabo sita na wasanii wa Bongo.

Hii maana yake ni kwamba rap style yake anahitajika sana Bongo?, kipindi cha nyuma rapper Chid Benz alikuwa akishirikishwa sana na wasanii wengi kutokana na aina yake ya uchanaji, je Bongo Flava anahitaji rapper mwingine aina ya Chid Benz?.

Chanzo: bongo5.com