Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makabila na mkewe wameachana tena

Makabila Sersss Makabila na mkewe wameachana tena

Tue, 15 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuachana na Mke wake Zaiylissa, kisha kupatanishwa tena na Zamaradi Mketema kwa kilao maalumu cha familia, Penzi la Dulla Makabila limekomonyoka tena ikiwa ni wiki moja tu tangu wapatanishwe.

"Nipo singo sipo kwenye ndoa na nipo tayari kuingia kwenye ndoa endapo nitampata Mwanamke atakayenielewa," amethibitisha Dulla Makabila.

Awali Zaiylissa alisema amepewa talaka tatu kwa mpigo ambazo zilipelekwa nyumbani kwao Mbagala Chamanzi zikiwa zimewekwa kwenye bahasha.

Aliongeza kuwa tangu waoane Dulla amekuwa na matukio ya rejareja na yasiyoisha ambayo ni pamoja na kufuma meseji za warembo wa mjini kwenye simu yake na akimuuliza anaambulia kipigo.

Mrembo huyo aliongeza kuwa si rahisi kuishi na mwanaume kama Dulla kwa sababu ana kashikashi nyingi na hata wakati anaolewa ndugu wa Dulla walimuita pembeni wakamwambia Dulla hajatulia awe naye makini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live