Menu ›
Burudani
Wed, 27 Dec 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mwanamuziki wa singeli nchini Dulla Makabila amedondosha list ya wasanii watano ambao hawana matatizo na mtu yeyote.
Makabila kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share picha ya wasanii watano ambao ni MwanaFa, Gnako, Barnaba, Mrisho Mpoto na Jaivah Striker huku akieleza kuwa ameona atumie muda kuwapongeza kaka zake ambao wameonekana hawana matatizo kwenye Tasnia na kuwataka wasanii wengine kujifunza kutoka kwa wakali hao.
Aidha, Makabila ameweka wazi kuwa ukiachana na list hiyo aliyoiweka muda siyo mrefu atakuja na list nyingine.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live