Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Makabila: Simuogopi Nay wa Mitego, namtaka aniombe radhi

Nay Makabila Nay wa Mitego na Dulla Makabila

Fri, 17 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii wa Singeli Bongo, Dulla Makabila amemjibu Nay wa Mitego baada ya Rapa huyo kutumia ukurasa wake wa Insta story yake kusema kuwa wasanii wengi wa Singeli hawajielewi huku akimtolea mfano Dullah makabila kuwa ni moja ya ambao hawajielewi,kichwani ni zero.

Hii inakuja baada ya msanii Makabila kuandika walaka mrefu sana wa kuomba radhi kwa msanii Diamond Platnumz ili amrejeshe tena kwenye familia ya Wasafi.

Kupitia Empire ya EFM, jana Juni 6, 2022, Makabila amedai Nay ni kaka yake lakini anapaswa kujua kuwa anamuheshimu na sio kuwa anamuogopa, hivyo anaweza kumvunjia heshima muda wowote na kama angekuwa na busara basi angemfuata private kumwambia amekosea na sio kwenda kumtukana hadharani mitandaoni.

Makabila pia amemtaka Nay wa Mitego amuombe msamaha haraka. Dullah ameongeza pia kwamba anaamini hakuna baya alilofanya na wanaoona amekosea wana chuki binafsi na Diamond.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live