Majizzo; ni CEO wa E-FM na TVE ambaye amekaa kwenye gemu la muziki kwa muda mrefu akiwa kama DJ ambaye naye ameingilia kati sakata la msanii Harmonize kumuomba msamaha Kajala Masanja au Mama Pau.
Majizzo ametumia kipande cha intavyu ETV ya Harmonize au Konde Boy akieleza namna alivyomkosea Kajala na familia yake na kuandika; “Okay suala la Konde, kwangu lina sura ya utu zaidi kuliko sura ya muziki (game) kama wengine wanavyoliona.
“Nje ya muziki na biashara, umaarufu na kila kitu, huyu ni mtu. Ni Rajabu, ana wazazi, ana moyo wa kupenda.
“Hii video imenigusa sana. Kanyoosha maelezo niliyokuwa nayakosa kutoka kwake na nadhani anafufundisha kitu;
“1; Binadamu mwenye uungwana, akitambua kosa lake anaomba msamaha. Harmonize alikosea na makosa yake yalienda public.
Alitakiwa kuomba msamaha, na ikibidi hadharani. Kafanya hivyo : Kwa nini atukanwe?
“2; Anaonesha kwamba anampenda Kajala kwa dhati, Je tutamhukumu kwa sababu ya kupenda?. Kila mtu ana namna yake ya kuelezea mapenzi yake, kwa kuwa hakosei mtu hastahili kejeli.
“Hapa palipofikia, anayeweza kumsaidia Harmonize amsaidie. Tusisubiri mabaya yamfike. Mimi nitajaribu kwa namna yangu na Kajala akitusikia na kuamua kusamehe nitashiriki kikamilifu ndoa yao.
“Harmonize umekua mdogo wangu, hongera ukomavu wa kuomba msamaha na kutaka kurekebisha ulipokosea. Pambania penzi lako.”
Kwa upande wake, Harmonize amemshukuru Majizzo; “Asante Kaka Mkubwa!”