Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majizo azungumzia ndoa yake na Lulu

89818 Majizo+pic Majizo azungumzia ndoa yake na Lulu

Thu, 26 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Umeshawahi kusikia kuhusu uchumba sugu?

Pamoja na mitandaoni kuwaita mastaa wawili Mkurugenzi Mkuu wa  EFM na tvE, Francis Ciza maarufu ’Majizo’  nyota wa filamu wa Tanzania Elizabeth Michael ‘Lulu’ ni wachumba sugu.

Kupitia mitandao ya kijamii ambako wamekuwa wakizongwa ni wachumba sugu wamejibizana kila mmoja anavyolichukulia suala la ndoa yao, huku Lulu akisema amekosa ndoa amepata pacha wake.

Lulu amekuwa mara kwa mara akiwajibu watu wanao mnanga kuhusu suala hilo mtandaoni, lakini kwa  Majizo hii ni mara ya kwanza kulijibu suala hilo.

Majizo leo Jumanne Desemba 24,2019 katika ukurasa wake wa  Instagram ameweka picha ya Lulu na kuandika ‘Nakukubali mshikaji wangu japo mwaka umeisha na ndoa haina dalili, lakini bado hujanikatia tamaa!. Nakukubali sana.”

Baadhi ya waliona ujumbe huo akiwamo Ms.shery amesema ‘”doa si kitu, kikubwa mnapendana hiyo inatosha na ndoa huwa haipangwi na watu subirini wakati wa Mungu.

">Wakati Ikupakyala yeye ameandika, “kwani shida nini, kanisani mbali au maana kama pesa ya ndoa bila mchango mnayo au nije kuwafungisha,”.

Adella Tillya's  ameandika “Nawakubali sababu mnaishi mnavyotaka sio watu wanavyotaka,”

Kutokana na ujumbe huo, Lulu naye alimjibu Majizo kwa kuweka picha yake aliyovalia nguo nyeupe aina ya pullover  na kuandika ‘Nakukubali Bro, Mswahili Numero Uno....tushakuwa ndugu tena maana umenipiga password mpaka tumeanza na kufanana..Yote kheri 2019 nimekosa wedingi nimepata Twin si haba. Nakukubali sana.”

Baadhi ya waliona ujumbe huo akiwamo akiwamo Steve Nyerere aliandika “nina mengi kausha hivyo hivyo...soon hutaamini wewe siyo wa kuvuta mzigo halafu ukaushe.”

Chanzo: mwananchi.co.tz