Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majizo aunda kamati kusaidia matibabu ya Ruge

42786 Pic+majizo Majizo aunda kamati kusaidia matibabu ya Ruge

Wed, 20 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kama ulidhani mkurugenzi wa kituo cha Radio EFM na E-TV, Francis Ciza maarufu ‘Majizo’ na Ruge Mutahaba walikuwa na uadui utakuwa unajidanganya.

Hii ni baada ya Majizo kuahidi kufanya jambo kwa ajili ya Ruge katika matibabu yake huku akidai kuwa Ruge, ambaye mkurugenzi wa vipindi wa Clouds Media Group si wa Clouds ni wa Watanzania.

Jana akiwa anahojiwa na Televisheni ya Clouds, kaka wa Ruge, Mbaki Mutahaba alisema mdogo wake katika matibabu hayo kwa siku hutumia si chini ya Sh5 milioni.

Akihojiwa leo Jumatano Februari 20, 2019 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na kituo cha Clouds TV, Majizo amesema tayari kamati ya kufanikisha uchangishaji wa matibabu hayo imeundwa na imeanza kukutana jana.

Amesema Watanzania watarajie kamati hiyo itafanikisha walilokusudia na kuwaomba wasiache kuwapa ushirikiano pale watakapowafuata kueleza walichoamua kufanya katika kufanikisha matibabu hayo.

“Lengo letu ni moja kuhakikisha Ruge anarudi mtaani kwani game bila yeye linakuwa halina ushindani, Watanzania tunapokuja kwenu tunaomba mtupokee, kwani Ruge ni wetu sote si wa Clouds tu,” amesema mkurugenzi huyo .

Akizungumzia uhusiano wake na Ruge, Majizo amesema ni kama rafiki, kaka na mshauri na kuongeza kuwa hata yeye alipofika hapo na kufungua kituo cha radio na TV ana mchango kwake.

Amesema Ruge ni mshindani mzuri wa kibiashara na kukiri kwamba unaposhindana naye yakupasa kuwa makini kwani ni mtu mwenye kufanya mambo kwa kutumia akili.

Pamoja na ushindani wake huo, amesema linapokuja suala la biashara na mambo binafsi huwa anaweka tofauti pembeni na kushauri vijana wa sasa kuiga mfano wao kwa kushirikiana.

“Mfano katika kampeni mwaka 2015, alinieleza kuwepo kwa fursa na kunishika mkono kunielekeza namna ya kuingia huko na ninashukuru nilifanikisha, hali ambayo kwa watu wengine ambao wana ushindani wa kibiashara ni ngumu kulifanya hilo,” alisema.

Wakati kuhusu suala la kufungua radio, amesema nalo lina mchango wake kwani pamoja na kukatishwa tamaa lakini alikuwa akimpa a,b,c za namna ya kulifanikisha.



Chanzo: mwananchi.co.tz