Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Majibu konki ya Lulu kuhusu hatma ya ndoa yake

Lulu+pic Majibu konki ya Lulu kuhusu hatma ya ndoa yake

Fri, 2 Oct 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By NASRA ABDALLAH OKTOBA mosi mwaka huu msanii mwenye tashtiti zake mjini, Elizabeth Michael maarufu Lulu, atakuwa amefikisha miaka miwili tangu alipovalishwa pete ya uchumba.

Pete hiyo alivishwa Oktoba mwaka 2018 na mchumba wake ambaye ni mfanyabiashara Francis Siza maarufu Majizo ambaye pia ni mmiliki wa EFM redio na TVE.

Ni kutokana na uchumba huo ambao baadhi wameuona ni wa muda mrefu amekuwa akikutana na maswali ya watu mbalimbali mtandaoni wakitaka kujua lini ataolewa huku wengine wakifika hatua ya kuukebehi kwa kuuita uchumba sugu.

Hii hutokea mara kwa mara hasa pale anapojipiga picha na kuweka kwenye ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram, ambao hadi kufika mwezi huu amefikisha wafuasi milioni tano.

Katika maswali hayo siyo mtu mmoja au wawili humuuliza kuhusu masuala hayo na bila kujali huwapatia majibu konki.

Katika makala haya tutakuletea maswali hayo na majibu yake hayo konki ambayo Lulu aliwahi kuwajibu watu wanaohoji uchumba wake huo, pete na mchumba wake Majizo.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz