Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maisha ya wanamuziki WCB kuwekwa hadharani

9561 Wcb+pic TZWeb

Wed, 20 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kipindi cha maisha halisi ya wanamuziki walio chini ya lebo ya WCB (The Real Life of Wasafi) kuanza kuonyeshwa wiki hii.

Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa uzinduzi wa chaneli ya Wasafi kuingia katika king’amuzi cha StarTimes, kiongozi wa WCB, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz amesema kipindi hicho kitaanza ikiwa ni zawadi yao kwa wateja wao.

Amesema, “Lengo la shoo hiyo ni kuonyesha walikotoka na ni kwa namna gani walipambana kufika walipo, na maisha yao ya kila siku.”

Meneja wa WCB, Tale Tale maarufu Babu Tale amesema kipindi hicho kitawapa nguvu vijana wengine wanaodhani mafanikio ya Wasafi yalikuja ghafla.

“Hii shoo itaonyesha kila kitu hadi wajomba zao waliopo vijijini, lakini pia itahusisha ziara na shoo zote za Diamond ikiwamo ya Marekani anayoianza wiki hii,” amesema Babu Tale.

Chanzo: mwananchi.co.tz