Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

SIL

Mahakama yavunja ndoa baada ya mke kunyimwa tendo miaka 7

Ndoa Zavubjika Dar.jpeg Mahakama yavunja ndoa baada ya mke kunyimwa tendo miaka 7

Fri, 27 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Mwanzo mkoani Mbeya imevunja ndoa ya Upendo Charles (40) na Nelson Sospeter(54) baada ya mke kudai kutopatiwa unyumba na mume wake kwa muda wa miaka saba.

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Asha Njovu, amaesema baada ya kusikiliza kwa kipa pande zote mbili Mahakama iligundua kuwa ndoa hiyo haitaweza kurekebishwa tena.

“Ndoa inarekebishwa na wau wawili yaani mume na mke, kadhalika ndoa hiyo inavunjwa na watu haohao yaani mume na mke” amesema Hamiku huyo.

Mbali na kunyimwa unyumba kwa kipindi cha miaka saba malalamikaji (Mke) amedai kuwa mume wake amemtelekeza pamoja na watoto wake bila kupatiwa huduma zozote za matunzo ikiwemo chakula, malazi na ada kwa ajili ya watoto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live