Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yasitisha tamasha la 'Wapi muziki na misosi'

IMG 20221012 WA0047 001 768x576 Nyama Mahakama yasitisha tamasha la 'Wapi muziki na misosi'

Sat, 26 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesitisha tamasha la 'Wapi Muziki na Misosi,' lililopangwa kufanyika kesho baada ya Master Chef Fred Uiso maarufu ‘Masapta Masapta,’ kudai kuwa jina lake limetumika kulitangaza tamasha hilo bila ridhaa yake.

Uiso ni mpishi maarufu, alifungua shauri hilo dogo la maombi namba 140 ya mwaka 2023 dhidi ya Kampuni ya EX NIHILO, Times FM Radio, Azam Media Group na Paul Mashauri akipinga wadaiwa hao kutumia jina lake, picha na umaarufu wake katika matangazo yao ya kibiashara yaliyolenga kuuhadaa umma kwamba Master Chef Fred Uisso atakuwepo kwenye tamasha hilo lililojulikana kama Wapi Muziki na Misosi.

Uamuzi huo umetolewa leo Agosti 25, 2023; na Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio, ambapo ameamuru, tamasha la ‘Wapi Muziki na Misosi’ lisitishwe na kwamba lisifanyike hadi haki za  mlakamikaji  kwenye kesi yake ya msingi namba 168 ya mwaka 2023 itakaposikilizwa.

"Tamasha hilo lililopangwa kufanyika hapo kesho katika viwanja vya Posta Kijitonyama, kuanzia saa mbili asubuhi, halitafanyika hadi kesi ya msingi ya mlalamikaji huyo itakaposikilizwa," amesema Hakimu Mrio.

Kwa upande wa mdai aliyewakilishwa na Wakili Ferdinand Makore, amedai kuwa mteja wake ni mpishi maarufu wa Kimataifa ambaye jina lake haliwezi kutumika na mtu yoyote katika suala lolote bila ridhaa yake.

“Kilichokuwa kinafanyika ni kuuhadaa umma na wapenzi wa tamasha hilo kuwa Master Chef Fred atashiriki katika tamasha hilo suala ambalo ni la uongo na wamefanya hivyo ili kupata turnover ya mashabiki wengi,” ameogeza Wakili Makore.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live