Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama yampata Tory Lanez na hatia ya kumpiga risasi rapa

Mahakama Yampata Tory Lanez Na Hatia Ya Kumpiga Risasi Rapa Mahakama yampata Tory Lanez na hatia ya kumpiga risasi rapa

Sun, 25 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Rapa Tory Lanez amepatikana na hatia ya kumpiga risasi mwanamuziki mwenzake wa hip-hop Megan Thee Stallion mwaka wa 2020.

Mahakama ya Los Angeles ilimtia hatiani Mkanada huyo mwenye umri wa miaka 30 kwa kosa la kutekeleza uzembe wa kufyatua risasi, kushambulia kwa kutumia bunduki na kubeba silaha iliyopakiwa na ambayo haijasajiliwa.

Anakabiliwa na kifungo cha zaidi ya miaka 20 jela.

Megan Thee Stallion, rapa mwenye umri wa miaka 27 aliyeshinda tuzo ya Grammy, awali alitoa ushahidi kwamba alipigwa risasi miguuni baada ya kuondoka kwenye tafrija.

Aliwekwa rumande na anatarajiwa kuhukumiwa tarehe 27 Januari.

Haikujulikana mara moja ikiwa alipanga kukata rufaa.

Akizungumza baada ya kesi hiyo kukamilika, mmoja wa mawakili wa Megan Thee Stallion aliwaambia waandishi wa habari ‘’majaji wamefanikiwa kufikia ukweli. Nashukuru Megan ametendewa haki.’’.

Chanzo: Bbc