Lifestyle

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

SIL

Mahakama yaamua amlipe mchumba'ke sh mil 6.3 baada ya kugoma kuolewa naye

COUPLEE Mahakama yaamua amlipe mchumba'ke sh mil 6.3 baada ya kugoma kuolewa naye

Fri, 27 Jan 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama nchini Uganda imeamuru mwanamke kumlipa mchumba wake wa zamani zaidi ya Shilingi milioni 10 za Uganda sawa na shilingi milioni 6.3 za Kitanzania kama fidia kwa kukiuka ahadi ya kuolewa na mchumba huyo.

Kulingana na jarida la Daily Monitor, Rekodi za mahakama zinaonyesha kuwa Richard Tumwine na Fortunate Kyarikunda, wote walimu walianza uhusiano wao wa kimapenzi mwaka wa 2015 na kwamba wawili hao baadaye waliweka ahadi ya kuoana mwaka wa 2018.

Mahakama pia ilisikiliza kwamba Tumwine, mwalimu wa Shule ya Msingi ya Kiringa, alimfadhili Kyarikunda- ikiwa ni pamoja na kumfadhili kwa stashahada ya sheria katika Kituo cha Maendeleo ya Sheria (LDC) ambapo alitumia zaidi ya Shilingi 313, 695.

Hakimu Mfawidhi wa Kanungu, Asanasio Mukobi alisema kwa kuwa ahadi ya kuoa haikutekelezwa na Kyarikunda na kumdhuru Tumwine. Bw Mukobi pia aliamuru Kyarikunda kulipa Sh33,770 kwa Tumwine kama fidia ya jumla kwa usumbufu na uchungu wa kisaikolojia.

Hakimu huyo aliendelea kusema kuwa Kyarikunda alipe gharama za kisheria alizotumia Tumwine katika kuendesha kesi yake.

"Ninaona, kutokana na kielelezo, miamala kadhaa ya kuhamisha pesa kutoka kwa simu ya mlalamikaji kwa majina ya Richard Tumwine kwenda kwa simu ya mshtakiwa kwa majina ya Fortunate Kyarikunda," hakimu alidhibitisha.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, Tumwine aliiambia mahakama kuwa sherehe za kutambulishwa kwake zilipangwa Februari 2022, lakini hazikufanyika bila sababu za msingi kutolewa.

Mahakama iliambiwa kwamba Kyarikunda alikuja na kisingizio ambacho wazazi wake wameeleza kuwa binti yao hapaswi kuolewa na mwanamume mkubwa akimaanisha Tumwine.

Lakini mahakama ilisema: “Hii pia haina maana, ni upotoshaji na ulaghai. Vyovyote vile, mshtakiwa alikuwa na fursa yote ya kukataa maombi ya upendo ya mlalamikaji mapema iwezekanavyo na kuepuka kuingilia majukumu yake ya kifedha.”

Mahakama iliona kwamba watu hao wawili walikuwa katika uhusiano wa kimapenzi na kwamba kutokana na maonyesho yaliyowasilishwa, mipango ya sherehe ya utambulisho ilifanywa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live