Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mahakama imetaja Tarehe itakayotoa Hukumu ya Kesi ya Masogange

Fri, 23 Feb 2018 Chanzo: millardayo.com

Leo February 15, 2018 stori ya Kimahakama nayokusogezea ni kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo inatarajia kutoa hukumu ya kesi ya kutumia Dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam inayomkabili mrembo Agnes Gerald ‘MasogangeFebruary 21, 2018.

Hatua hiyo inatokana na Masogange kufunga ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ambapo aliongozwa na Wakili wake Nehemia Nkoko.

Katika ushahidi wake mbali na mambo mengine Masogange amedai kuwa hajawahi kutumia Dawa za Kulevya, hivyo anaiomba Mahakama imuachie huru kwa sababu hana kosa.

Masogange anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 katika maeneo yasiyojulikana ndani ya jiji la Dar es Salaam alitumia Dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine).

Pia anadaiwa kuwa kati ya February 7 na 14, 2017 alitumia Dawa za kulevya aina ya Oxazepam.

BREAKING: POLEPOLE ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI, BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUTAZAMA

Chanzo: millardayo.com