Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Magreth Yohana Magreth ndiye anayeigiza sauti ya Afife Hatun katika tamthilia hii.

Tue, 22 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Ni tamthilia inayohusu maisha ya Sultan Suleyman. Katika umri wa miaka 26 alianza mbio za kuitengeneza himaya yake ya Ottoman akitaka iwe kubwa kuliko ya Alexander the Great.

Kuhusu Afife Hatun

Katika tamthilia hii Afife Hatum ni bibi ambaye kapewa jukumu la kulea na kufundisha adabu watu wanaokaa kwenye kasri ya Sultan.

Pia bibi huyu ndiye mama wa Yahya Efendi, kijana aliyelelewa na wazazi wa Sultan Suleiman katika makuzi yake.

Kati ya watu ambao Afife amekuwa akiwasimamia ni pamoja na wake wa Sultan, Hurrem na Mahidevran, ambao katika maisha yao kila mmoja anavutia kwake ili apendwe na kupata maisha bora kuliko mwenzie.

Nafasi hii imechezwa na Sabina Toziya, aliyezaliwa mwaka 1946 nchini Macedonia, ni mwigizaji aliyeanza kufanya kazi hiyo tangu mwaka 1984.

Mara ya kwanza Sabina alionekana katika filamu ya Opasni trag na baadaye ile ya Salon Harmoni aliyoicheza mwaka 1998 na nyinginezo.



Chanzo: mwananchi.co.tz