Nyaraka za Mahakama zimethibitisha kuwa rapa Sean Diddy Combs alitumia mafuta ya watoto yaliyowekwa dawa aina ya GHB (Gamma hydroxybutyrate) inayojulikana kama 'date rape drug' kutekeleza njama zake
Kwa Mujibu wa Daily Mail, Mashtaka sita mapya yaliyowasilishwa wiki hii dhidi ya Diddy yote yalidai kutumika dawa hiyo ambayo huja katika hali ya kimiminika ambayo inaweza kufyonzwa kwenye ngozi na kurahisisha waathirika kushambuliwa.
Yaliyomo kwenye chupa 1000 zilizokamatwa miezi kadhaa kwenye nyumba za Diddy za Miami na Los Angeles yanalingana na taarifa za awali zilizotolewa kuhusu dawa hizo na Damian Williams, Mwanasheria wa huko New York, Marekani.