Vazi alilovaa mwigizaji kutoka nchini India Alia Bhatt kwenye tamasha la mitindo duniani ‘Met Gala’ lililofanyika siku ya Jumatatu Mei 6 katika ukumbi wa ‘Metropolitan Museum of Art’ Manhattan, New York City, nchini Marekani ladaiwa kutengenezwa na mafundi 163.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa #Alia alieleza jinsi vazi hilo lilivyobuniwa ambapo aliweka wazi kuwa lilitengenezwa kwa mikono nchini India na timu ya mafundi 163 huku likichukua takribani saa 1965 kukamilika.
Vazi hilo lenye asili ya kihindi lilibuniwa na mbunifu kutoka nchini India aitwaye ‘Sabyasachi Saree’ ambapo kwa mujibu wa maelezo yake aliweka wazi kuwa ili kunogesha zaidi ilimbidi atumie timu kubwa ya watu pamoja na kuongezea vito vya thamani katika nguo hiyo.
Hii si mara ya kwanza vazi la #Sabyasachi kuonekana kwenye ‘Met Gala’ mwaka 2022 alibuni gauni la mfanyabiashara Natasha Poonawalla.
#Alia Bhatt (31) ameonekana katika filamu kama ‘Rocky Aur Rani Kii Prem Kahaani’, ‘Student of the Year’, ‘#Brahmāstra’, ‘#Darlings’, ‘Heart of Stone’ na nyinginezo.
Aidha watu maarufu wengine kutoka nchini India ambao wamehudhuria kwenye ‘#MetGala2024’ ni Isha Ambani, Natasha Poonawalla, Sudha Reddy, Mona Pate na wengineo.