Burudani

Habari

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mafufu: Huyu hata sipimi DNA, mleteni!

Jimmy Mafufu279364 Mafufu: Huyu hata sipimi DNA, mleteni!

Mon, 10 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msanii maarufu wa Bongo Movies, Jimmy Mafufu amefunguka kuhusu picha na maneno yanayosambaa mitandaoni kuhusu kijana anayedaiwa kuwa ni mtoto wake aliyezaa na mwanamke nchini Uganda miaka ya nyuma kisha kumtelekeza huko.

"Picha zinasambaa sana mitandaoni, sikutaka kusema lakini acha niseme kidogo, taharuki ni kubwa sana watoto wangu wameona picha hizi na zimewastua kusema za ukweli, hata mimi nimestuka sana kumuona mtu kama mimi nitoe taarifa rasmi kwamba huyu kijana simfahamu lakini nasikia yuko Uganda.

“Yes wakati naanza kujishughulisha na mambo ya mizagamuo mwanamke wangu wa pili kukutana nae alikua anatokea Uganda siwezi kumkumbuka hata kwa sura lakini nakumbuka nimewahi kuzitikisa chaga na Muganda mmoja mrembo mashaalah, lakini hiyo haitoi fursa kwamba nilimpa mimba au huyu ni mwanangu.

“Wwadaku vema mumtafute huyu kijana awaeleze baba yake ni nani kama ni mwanangu nitampokea na matarumbeta siachagi mtoto wangu popote labda mama yake amzuilie kwa nguvu sintakua kama Mzee Yusuf.

“Yaani akisema mimi ni baba yake hata DNA sitaki, mleteni nyumbani aendelee kula ugali na wenzake maana mimi naamini watoto ni baraka kutoka kwa Mungu, nasisitiza simjui huyu kijana nyie waandishi mnaonipigia simu mtafuteni mupate ukweli akiwaambia nahusiaka wala msipate tabu, nileteeni nitampokea kwa mikono yote miwili na sherehe ya welcome hom son nitamfanyia, Mungu awabariki sana wote mliopatwa na usumbufu huu,” amesema Mafufu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live